Sunday, June 22, 2008

JE UNAJUA NGUVU YA AGANO.

Agano ni kitu ambacho MUNGU alikianzisha ili kuwepo na muungano kati ya pande mbili tofauti,ushirikiano na upendo kwa marafiki wa kweli.Nitakuonyesha aina 3 kubwa za maagano ingawa zipo nyingi:-

AINA TATU ZA AGANO.
  • AGANO LA MUNGU NA MWANADAMU BINAFSI:-kwetu sisi ambao ni wakristo tunaamini kuwa MUNGU alianza kufanya agano nasi toka kale kwanza alianza na adamu na hawa,hapa alifanya agano nao binafsi pale walipoasi,MUNGU alipoona tayari Adamu na Hawa wamemuasi,japokuwa aliwaazibu lakini bado alitaka agano nao,ndipo MUNGU akalazimika kuchinja kondoo na kuwaambia wavae ngozi ya kondoo.Hapo unaweza ukanitega na kusema sasa Zablon mbona hayo ni mavazi walitengenezewa?,nitakujibu kwa kukuuliza swali mbona walitengeneza majani wakajifunika nayo,lakini hawakutosheka nayo, na tena mbona kabla ya kuasi hawakuchinja kondoo wakajifunika?,na mbona baada ya kuasi walichinja kondoo na si mbuzi?.Jibu ni MUNGU alitaka damu imwagike,na alitumia kondoo akimaanisha baadaye atamleta YESU (ambapo kwa kukuhakikishia YESU alivyokuja duniani,walimuita mwanakondoo wa MUNGU) . Pili ni MUNGU na wana Israel, hapa ilitokea pindi wana wa Israeli walipokuwa wanateswa sana na Wamisri MUNGU aliwaambia wachinje kondoo na wapake damu juu ya milango yao,na kitendo hiko wafanye kwa siri.Mh kweli Malaika wa MUNGU alipita akaangamiza wazawa wa kwanza wote wa Wamisri kuanzia wanadamu hadi mifugo.Tatu ni Agano la YESU na wanadamu wote alivyomwaga damu pale aliposulubiwa msalabani,na kusababisha sasa watu waweze kuokoka.
  • PILI NI AGANO BAINA YA MKE NA MUME:- Hapa watu wengine watanichukia lakini ndio kweli,unajua MUNGU aliweka tendo la ndoa liwe kwaajili ya wana ndoa tu.Kusudi lake lilikuwa Bibi harusi akiolewa akiwa bikra na bwana harusi akawa hivyo hivyo,wakiwa kwenye tendo la ndoa msichana kunalea ya ngozi itachanika na bwana harusi atapata mchubuko ambapo damu itaungana na kufanyika agano la kutokutengana mpaka mauti.Nakupa zoezi wewe mwenye jinsia kama yangu kama ukiweza kumuuliza msichana ambaye hatakuficha ukweli,umuulize je amemeweza kumsahau yule aliyemtoa bikra,au kwa wewe msichana je umeweza kumsahau aliyekutoa bikra (hiki ni kidhibitisho tosha kudhibitisha hili).Na kwa wavulana hivyo hivyo
  • TATU NI AGANO BAINA YA MAMA NA MTOTO:-Hapa kila mtu anajua mtoto anavyozaliwa,hakuna jinsi madaktari watakavyofanya wamzalishe mama mjazito bila damu kutoka iwe kwa njia ya operation au ya kawaida.Ndio maana hata kama mtoto atamuudhi vipi mama yake,bado mama ana doa la upendo wa dhati kwa mtoto,lakini si baba (sorry washikaji zangu tulio jinsia moja,penye ukweli tuseme ukweli).

USHAURI

Tutubu kwa MUNGU tukimaanisha kubadilika na kumpokea YESU awe bwana na mwokozi wetu,nakukuhakikishia agano lake hufunika maagano yote yaliovunjika.TUACHE UBISHI MUNGU YUPO NA WOKOVU UPO.